Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PROIN PROMOTIONS YAANZA RASMI KUTAFUTA VIPAJI.

PROIN PROMOTIONS YAANZA RASMI KUTAFUTA VIPAJI.

Kampuni inayojishughulisha na utengenezaji na Usambazaji wa Filamu hapa Tanzania ‘Proin Promotions’ sasa yapiga kambi jiji la Mwanza kwa ajili ya kusaka vipaji.
Proin Promotions Limited ni kampuni iliyokuja kwa kasi na kupata mafanikio kutoka na kazi wanazozisimamia kuwa na ubora wa juu.
Kwa sasa kampuni hiyo imekuja na kitu kipya cha kusaka vipaji inayofahamika kwa jina la ‘Tanzania Movie Talents’ na sasa ipo jijini Mwanza ikiendelea usakaji wa vipaji vya kuigiza filamu meneja wa masoko wa Proin Promotions Bw. Evance Stephen aliongea na mwandishi wa Baabkubwa na kusema.
“Proin Promotions Team tupo tupo Mwanza na tunaendelea na mchakato wa kumtafuta mshindi wa ili aweze kuungana na wenzake katika mikoa mingine na mshindi wa kanda ya ziwa anatarajia kupatikanika siku ya kesho, jumapili na baada ya hapo tutaelekea katika kanda zifuatazo ,kanda ya kati Dododma, kanda ya kaskazini Arusha, kanda ya juu kusini Mbeya, kanda ya kusini mashariki Mtwara na special zone Kigoma, na baadae kuingia kambini Dar es Salaam.” Evance alisema
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Chapisha Maoni

CodeNirvana
© Copyright J MarcoBlog
Back To Top